October 20, 2018



BAADA ya kurejea juzi usiku, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewapa onyo wachezaji wake kwa kuhakikisha wanatumia akili nyingi watakapovaana na Alliance leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Yanga ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 16 wataivaa Alliance kutoka Mwanza yenye alama sita katika mchezo namba 94 wa ligi kuu.

Akizungumza na Championi Jumamosi, kocha huyo alisema mchezo huo hautakuwa rahisi hivyo wachezaji wake ni lazima watumie akili katika kupambana ili waweze kupata matokeo mazuri.

“Unajua nimewaambia wachezaji wangu kuwa kama tunahitaji kushinda mechi na Alliance ni lazima wawe makini katika uchezaji wao na watumie akili ya ziada sababu haitakuwa mechi rahisi hata kidogo.

“Sababu tunahitaji kushinda mchezo huo na wenzetu kama unavyofahamu watapambana kweli ili kuweza kupata matokeo jambo ambalo litafanya mchezo kuwa mgumu lakini tutapambana tu,” alisema Zahera.

Katika mchezo huo, Yanga itamkosa Vicent Andrew ‘Dante’ kwenye kikosi hicho kutokana na kufungiwa mechi tatu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kumpiga kichwa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba pindi timu zao zilipokutana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic