TAIFA STARS YAWASILI KINYONGE DAR
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imewasili jioni ya leo ikitokea Cape Verde kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Africa 2019.
Katika mchezo huo, Stars ilikubali kuchapwa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji nchini kwao.
Kikosi hicho kimekwenda moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo wa Jumanne Oktoba 16, 2018.
Stars itarudiana tena na Cape Verde katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment