Ni katika Kipindi cha Nyundo ya Baruan Muhuza ambapo Alhamisi hii Msemaji wa Simba Haji Manara ndiye aliyekuwa mgeni, amefunguka mengi ikiwemo kupinga kauli ya Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera baada ya mchezo wa #WataniWaJadi kati ya Simba na Uliopigwa Septemba 30, 2018 kwenye Uwanja wa taifa Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
Mengine aliyozungumza ni pamoja na kukataa Yanga wasiitwe mabingwa wa kihistoria, asema Simba ndiyo inayoongoza kwa makombe Tanzania.
Asema ndoto yake ni kuwa Rais wa Tanzania katika miaka ijayo.
Azungumzia mgawanyo wa mapato kwenye mechi ya Simba na Yanga iliyopigwa Septemba 30, 2018.
Afunguka mapya kuhusu mtifuano uliopo kati ya kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems na Kocha msaidizi Masoud Djuma.
Asisitiza takwimu kuwa Simba ndiyo inayoongoza kwa makombe mengi Tanzania kuliko Yanga.
Asema atakachofanya ili mitandao ya kijamii ya Simba iwe na nguvu zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment