October 13, 2018


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,  leo amesema nchi ipo salama na Watanzania waendelee na shughuli zao za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwani serikali imejipanga vizuri katika kushughulikia matukio yote ya uhalifu yanapojitokeza.

Lugola ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipoongea na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam aliposisitiza kwamba mpaka sasa watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi kufuatia tukio la kutekwa mfanyabiashara na mwekezaji katika Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji) katika gym ya Hoteli ya Colosseum, Oyster Bay jijini Dar es Salaam.

“Sababu ya kutekwa kwa MO itafahamika pale tu jeshi la polisi litakapompata yeye na kueleza kisa cha kutekwa kwake,” alisema na kuongeza kwamba hilo litafahamika kirahisi endapo watekaji watakamatwa na kubanwa kuelezea juu tukio hilo.

Watanzania wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu na kuacha kusambaza habari zisizo za kweli na kwamba taarifa zozote zinazohusu matukio, yakiwemo ya upoteaji wa watu zitatolewa na mamlaka za serikali ikiwemo Jeshi la polisi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic