October 19, 2018



Kocha mkuu wa timu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema atafanya maamuzi magumu kwa  wachezaji wake wote ikiwa ni pamoja na Herrieter Makambo,Ibrahim Ajibu  kwa kuwatoa uwanjani endapo watakuwa wavivu .

Zahera amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Alliance ni muhimu kwao kupata ushindi na amewaambia wote mechi ni ngumu kuliko ile ya Simba.

"Tupo tayari wachezaji wote wazima wana morali,  lengo kubwa ni kupata ushindi, nimewaambia kuwa naiogopa sana mechi hii zaidi ya ile ya Simba  .

"Mchezaji atakayedharau mchezo  kwa kufanya uvivu uwanjani nitamtoa ndani ya dakika 10 na kumuingiza mchezaji mwingine ni mchezo muhimu sana" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic