November 19, 2018


Beki wa timu ya Prisons ya Mbeya, Salum Kimenya amesema kuwa yupo tayari kujiunga na Simba ili kusaidiana majukumu na beki Shomari Kapombe endapo uongozi utakubaliana na matakwa yake.

Uongozi wa Simba unamtaka Kimenya ili asaidiane majukumu na Kapombe ambaye inadaiwa atakuwa nje kwa muda wa miezi mitatu kutokana na kuumia mguu akiwa na Stars Afrika Kusini.

"Taarifa za kuhitajiwa na Simba nimesikia na kuna baadhi ya viongozi wa Simba nimewasiliana nao ila kuna mambo nimewaeleza ili wayatimize kwanza kama kweli wanataka nikaitumikie.

"Mimi ni mwajiliwa wa Jeshi la Magereza kwa hiyo kuna vitu ambavyo kabla ya kufanya maamuzi magumu lazima niwe na uhakika navyo nisije nikajutia," alisema.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameagiza uongozi ufanye usajili makini kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye timu kwa nafasi mbili ambazo hazina mbadala ndani ya kikosi.


2 COMMENTS:

  1. hana uwezo wa kuingia moja kwa moja kwny team hyooo,then wachezaj wa prisons wanaznguaga sana kuja Simba, sio mara ya kwanza kuwataka Chona,beno,kimenya,Henry Morris,Dennis Edwin tmf

    ReplyDelete
  2. huyu alidengua mwanzoni kaona timu imenoga anaanza kujipigia debe utasikia mchezaji anataka milioni 50 wakati uwezo wake ni mdogo haulingani na thamani ya pesa anayopewa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic