November 19, 2018


Kiungo mshambuliaji wa Yanga mwenye rekodi ya kufunga 'Hat-trick' kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mrisho Ngassa amepata kigugumizi kumtaja mshambuliaji wa Simba kati ya Emmanueli Okwi, Meddie Kagere na John Bocco kuweza kuvunja rekodi.


Ngasa alifanikiwa kuweka rekodi hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwafunga Etoile d'Or 2009 na klabu ya Komorozine nje ndani 2014 zote za kutoka Comoro ameshindwa kumtaja mshambuliaji wa Simba ambaye anaweza kuvaa viatu.


Ngassa amesema kuwa aliweza kufanikiwa kufanya vizuri katika mashindano hayo akiwa ndani ya Yanga kutokana na kujituma pamoja na ushirikiano mzuri uliokuwa ndani ya kikosi.

"Mchezo wa mpira unakanuni nyingi ambazo inabidi zifuatwe ila kwa kuweza kuzungumzia kwa sasa atakayeweza kuvunja rekoodi yangu bado sijamjua kwa kuwa ni jambo kubwa na ili kuweza kuzungumzia ni lazima uwe umetulia kwa muda," alisema.


Simba itawakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ambapo watacheza na Mbabane Swallows FC ya nchini Swaziland Novemba 28 Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic