Uongozi wa timu ya Yanga umemfuata beki wa Mtibwa Sugar, Rojas Gabriel mwenye uwezo wa kucheza zaidi ya nafasi mbili uwanjani.
Rojas Gabriel amesema kuna viongozi wa Yanga ambao wamemfuata na kuzungumza naye ili ajiunge nao kwenye dirisha dogo kusaidiana na Paul Godfrey pamoja na Juma Abdul.
"Kuna viongozi wa Yanga wamenifuata na kunitaka ili niweze kujiunga nao kwa kuwa wamekubali uwezo wangu hasa kwa nafasi ambayo nacheza uwanjani, hivyo nimewapa masharti wakiyatimiza nitajiunga nao kwa kuwa kazi yangu ni mpira.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kamati ya ya Usajili ya Yanga, Hussen Nyika alisema kuwa wanatambua kuwa lazima wafanye usajili makini kwenye dirisha dogo hivyo hawahitaji papara watafuata maelekezo ya mwalimu.
"Hakuna ambaye anapenda kikosi chake kushindwa kupata matokeo, tumejipanga kufanya usajili makini hivyo mashabiki watulie mipango ikikamilika tutatangaza wachezaji ambao tutawasajili kupitia ripoti," alisema.








0 COMMENTS:
Post a Comment