November 23, 2018


Imeelezwa kuwa Kocha mpya wa klabu ya Black Leopards ya Kenya, Dylan Kerr, amewataka mabosi wake wamsajili kiungo wa Gor Mahia FC, Francis Kahata ili kuipa makali timu hiyo.

Kerr ameamua kuutaka uongozi wa timu hiyo ufanye usajili wa Kahata ambaye anamwani atakisaidia kikosi chake kuelekea mbio za ubingwa msimu huu.

Kerr amemtaja Kahata ambaye pia imeelezwa anawaniwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba Sports Club ya Dar es Salaam.

Simba imeanza kutajwa miezi kadhaa iliyopita kuwa inahitaji saini ya mchezaji huyo ili kuja kuongeza nguvu kwenye safu ya kiungo haswa kuelekea Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tayari dirisha dogo hapa nchini limeshafunguliwa na mpaka sasa wekundu hao wa Msimbazi hawajasajiri mchezaji hata mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic