Mshambuliaji wa timu ya Azam, Donald Ngoma ambaye alisajiliwa akitokea Yanga, amelivuruga benchi la ufundi kutokana na kadi nyekundu aliyopata katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar hivyo kushindwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza na Ruvu Shooting Novemba 22.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddy Cheche amesema kuwa Ngoma ni mchezaji mzuri ambaye anauwezo wa kubadilisha matokeo ila watamkosa katika mchezo wao ujao kutokana na adhabu aliyonayo hali itakayowafanya watafute mbadala wake.
"Tayari alishaanza kuonyesha makali yake ambayo tuliyatarajia ila kutokana na adhabu yake ya kadi nyekundu ataukosa mchezo ujao, sasa tutakachofanya ni kutumia mchezaji mwingine kwani kwa sasa tuna kikosi kipana chenye wachezaji makini," alisema.
Ngoma amefanikiwa kufunga mabao 3 kwa sasa baada ya kurejea kwenye hali yake alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti, jukumu lake kubwa uwanjani alilopewa ni kufunga na kutengeneza pasi ya bao.
0 COMMENTS:
Post a Comment