DE GEA, RAMSEY, BAILLY, DE JONG, DE LIGHT: TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI
Manchester United itatoa ofa ya pauni ya milioni 60 kwa akipa wa Everton wa miaka 24 Jordan Pickford ikiwa Mhispania David de Gea, 28, hatakubali kuongeza mkataba wake. (Sun on Sunday)
Manchester City wamewashinda Barcelona katika mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Ajax raia wa uholanzi mweye miaka 21 Frenkie de Jong. (Sunday Mirror)
Liverpool wanatarajiwa kumsaini kiungo wa kati wa Hoffenheim Mjerumani Kerem Demirbay, 25, mwezi Januari (Sunday Express)
Lakini matumaini ya Liverpool kumsaini mlinzi wa Ajax anayewekewa thamani ya pauni milioni 60 Matthijs de Ligt yanaaonekana kufifia baada ya mchezaji huyo wa miaka 19 raia wa uholanzi kuhusishwa na Barcelona. (Sunday Mirror)
Paris St-Germain wamejiunga kwenye mbio za Arsenal na Tottenham kumwinda mlinzi wa Manchester United mwenye miaka 24 raia wa Ivory Coast Eric Bailly. (Mail on Sunday)
Kiungo wa kati wa Arsenal na wales Aaron Ramsey, 27, atalipwa pauni milioni 10.4 ikiwa atahama kwenda Juventus. (Sun on Sunday)
Manchester United, Chelsea, Liverpool, Tottenham na Manchester City wanamfuatilia kiungo wa kati wa Brazil Bruno Roberto ambaye ameingia kikosi cha kwanza cha Atletico Mineiro. (Mail on Sunday)
Mlinzi wa Manchester United na Englans Ashley Young, 33, yuko tayari mshahara wake kupunguzwa kubaki Old Trafford. Mkataba wake wa sasa unafikia mwisho msimu huu. (Sun on Sunday)
Mlinzi Antonio Valencia analenga kujiunga na klabua nyingine ya Ligi ya Premier ikiwa hawezi kukubaliana na Manchester United. Mchezaji huyo wa miaka 33 raia wa Ecuador mkataba wake utakamimilika msimu wa joto. (Metro)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumleta beki wa West Ham na Jamhuri ya Ireland Declan Rice, 19 huko Old Trafford. (Daily Star Sunday)
Mourinho pia anamfutilia mlinzi wa Brighton mwenye miaka 27 Lewis Dunk, ambaye aliichezea England siku ya Alhamis dhidi ya Marekani. (Sunday Express)
Chelsea haitamzua Ruben Loftus-Cheek ikiwa mchezaji huyo mwenye miaka 22 raia wa England atataka kuondoka. (Daily Star Sunday)
Liverpool wamejiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Fabinho, 25, kupata pesa za kummnunua wing'a wa Borussia Dortmund na Marekani Christian Pulisic ambaye pia analengwa na Chelsea. (Sunday Mirror)
Mshambuajia raia wa Venezuela Salomon Rondon, 29, anataka kuhama kabisa kutoka West Brom kwa mkopo kwenda Newcastle. (Chronicle)
Beki wa zamani Mfaransa Patrice Evra anatarajia kurudi Manchester United wajibu wa ubalozi. (Mail on Sunday)
Manchester United bado wanataabika kufuatia kustaafu kwa meneja Sir Alex Ferguson, anasema mchezaji wa zamani raia wa Argentina Juan Sebastian Veron. (Marca)
Manchester City wanampango wa kuongeza uwezo wa uwanja wa Etihad kuchukua hadi watu 63,000 na wamekutana na mashabiki kuzungumzia mpango huo. (Mail on Sunday)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment