November 18, 2018


Na George Mganga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli, amemwagiza Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe kwenda kuwapa morali ya nguvu Taifa Stars.

Mwakyembe ambaye yuko Lesotho hivi sasa ameagizwa na Rais Magufuli kuipa hamasa Stars ili iweze kushinda na hatimaye kujipatia tiketi ya kufuzu kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika huko Cameroon mwaka ujao.

Waziri Mwakyembe amesema Rais Magufuli haoni sababu ya Stars kutopata matokeo leo dhidi ya Lesotho kutokana na namna maandalizi kwa ujumla yalivyofanyika.

Ameeleza kuwa Rais Magufuli amemwagiza awaambie vijana wapambane ili waitangaze nchi vizuri na iweze kupata nafasi hiyo baada ya kuikosa kwa miaka mingi.

"Rais Magufuli amesema hakuna haja ya sisi kushindwa kupata matokeo, ni lazima twende AFCON, tunawataka wachezaji wetu waoneshe umoja na nguvu uwanjani ili tuweze kushinda mechi dhidi ya Lesotho.

Ukiachana na Taifa Stars, timu za Lesotho, Uganda na Cape Verde nazo zipo kwenye kundi moja 'L' wakati Uganda tayari wakiwa wamefuzu baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cape Verde hapo jana.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki pamoja na wadau wengi wa soka hapa nchini itaanza majira ya saa 11 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic