November 23, 2018


Kocha wa timu ya Lipuli FC, Seleman Matola amesema wanaimani ya kuweza kuwasimamisha Simba katika uwanja wao wa nyumbani mbele ya Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.


Lipuli FC watacheza na Simba leo katika mchezo wa ligi kuu msimu huu, huku Lipuli wakiwa na mwendo wa kusuasua kutokana na kuyumba kiuchumi.


 Matola amesema anatambua kikosi cha Simba ni kizuri ila atatumia uzoefu wake kuhakikisha anaweza kupata matokeo mbele ya wachezaji ambao wana juhudi za kutafuta matokeo.

"Hatuchezi na mchezaji mmoja ama wawili sisi tumejipanga kwa ajili ya kucheza na timu na tutafanya kweli kwa kuwa nawatambua vizuri wachezaji wa Simba na uwezo wao pia nautambua.


"Mbinu ambazo nimewapa wachezaji zitawafanya waweze kupata matokeo licha ya hali ambayo tunapitia naamini kila kitu kitakuwa sawa, hivyo wadau waendelee kutupa sapoti," alisema Matola.


Msimu uliopita Simba walipata taabu kuwafunga Lipuli kwani katika michezo yote miwili waliyocheza walitoka sare ya kufungana mabao 1-1.

6 COMMENTS:

  1. Huo ni msimu uliopita ngoja uone mvua ya mabao itakayoshuka Leo,waombe mungu chama na okwi wasicheze.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wew ndo boya Kwan anacheza chama na okwi tu wanna mzima?

      Delete
  2. Boya atajulikana baada ya mechi,punguza povu kijana hapa ni jukwaani,lazima mpigwe maana hakuna namna.

    ReplyDelete
  3. Kaa ukijua katika mchezo wowote kuna wahusika wanakua ndio mihimili,mfano umeuona juzi kilichotokea south,wala usijitoe ufahamu ndugu yangu.

    ReplyDelete
  4. Kaa ukijua katika mchezo wowote kuna wahusika wanakua ndio mihimili,mfano umeuona juzi kilichotokea south,wala usijitoe ufahamu ndugu yangu.

    ReplyDelete
  5. Boya atajulikana baada ya mechi,punguza povu kijana hapa ni jukwaani,lazima mpigwe maana hakuna namna.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic