November 14, 2018


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imebadilisha ratiba ya kusikilizwa kwa kesi za aliyekuwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva pamoja na aliyekuwa Makamu wake, Godfrey Nyange Kaburu.

Mahakama hiyo imeamua sasa kesi hiyo kusikilizwa mfululizo katika tarehe za Novemba 26, Disemba 4 na 5 mwaka huu.

Wawili hao mpaka sasa upelelezi wa kesi yao haijakamilika ambapo juhudi za mahakama kuendelea na harakati za kuukamilisha bado unaendelea.

Wawili hao wanatuhumiwa na makosa ya ubadhirifu wa masuala ya fedha jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.

Pia aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hanspope, naye aliunganishwa kwenye kesi hiyo japo yeye ana dhamana ya kuwa nje ya mahabusu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic