WALIOCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA YANGA MPAKA SASA HAWA HAPA
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, amechukua fomu ya kugombea Uenyekiti ndani ya klabu hiyo jana.
Tiboroha amefikia maamuzi hayo akiamini anaweza kuwa chachu ya mabadiliko ndani ya Yanga na kuamua kuchukua fomu hiyo.
Mwanachamu huyo ambaye aliwahi kuwa kiongozi ndani ya Yanga miaka kadhaa nyuma na baadaye kuelekea Stand United, amekuwa mtu pekee aliyechukua fomu hiyo.
Halikadhalika katika upande wa Makamu Mwenyekiti, Yono Kevela naye amechukua fomu hiyo.
Kwa upande wa Wajumbe waliochukua fomu ni pamoja na Hamad Ally, Benjamin Jackson, Silvestoer Haule, Musa Katabaro,Said Baraka, Pindu Luhoyo, Dominic Francis na Jeko Jihadhari.
0 COMMENTS:
Post a Comment