Kikosi cha timu ya Simba kimekubali sare ya kutofungana na timu ya Lipuli FC kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wapo kwenye kibarua kizito cha kuvunja rekodi ya Matola ambaye msimu uliopita kwenye michezo yote miwili alifanikiwa kutoka sare za kufungana baao 1-1 na leo ameanza kwa kutoa sare ya bila kufungana.
Mchezo huo ambao timu zote zilikuwa zinashambuliana kwa zamu na washambuliaji wakikosa nafasi za wazi kwa kukosa umakini.
Kwa matokeo hayo Simba inakuwa na Pointi 27 ikiachwa kwa pointi 2 na Yanga wenye pointi 29 wakiwa nafasi ya pili huku Azam FC wakiwa nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 30.







Simba hakuna Kocha huyo ni mtalii.. Kikosi ghali kinatoa droo na wachezaji wasio hata na uhakika wa kula. Haya ni maajabu saba ya Dunia.. Kwa Kocha huyu hata hao Mbabane Swallow watatupiga nje ndani... FUKUZENI HUYU KOCHA BADO MAPEMA VINGINEVYO MAJUTO NI MJUKUU..
ReplyDeleteHa ha ha povu mapema ivyo !?kwan mmeumbiwa kushinda nyinyi tu ?tulien huo ndio mpira
DeleteKwa uchezaji aliocheza Mkude leo wakati mwingine unawaza may be Amunike is right,mwisho wa siku unaona kuwa kama Taifa mpira bado.
ReplyDeleteAmeanza lini kuwa mtalii?
ReplyDeleteWewe unaesema kocha ni mtalii afukuzwe Simba kwa kutoa sare,hapana shaka utakuwa una ushoga wa akili. Hivyo hujawahi kusikia Baercelona au Real Madrid hata wakati wa zedani wakifungwa na vitimu vya ajabu ajabu pale Spain? Kitimu kama lipuli kikicheza na Simba kuanzia kocha wao mpaka wachezaji wa akiba wanachoangalia ni kucheza jihadi na kukamia ili kuonekana pale Simba kwa ajili ya kupata ajira na ikishamalizika mechi ya Simba basi wanakwenda kufungwa na biashara ya mara timu inayoshika mkia.
ReplyDeleteYanga tuliyaongea haya haya dhidi ya Ndanda mkatuambia hamna kitu
DeleteMpira wa jana jamani acheni tu, kuna wakati nilikuwa natukana peke yangu baada ya kuwaona akina Boko, Kagele na Mohamed wakikosa magori ya kugusa. Binafsi sielewi ni kwanini, ila wazi jana kiungo tulizidiwa, kipindi cha kwanza beki ilikuwa haina mawasiliano mazuri, na pia kulikuwa hakuna muunganiko kati ya beki kwenda kwa viungo. Zaidi katika mpira ambao wamewahi kuucheza Simba msimu, mechi ambayo ilikuwa na makosa mengi ya beki na washambuliaji, ni hii ya jana. Kiukweli jana Simba mlinifanya nimfokee mwanangu bila sababu ya msingi. Kocha, kama huwa unasoma comments hizi, jana umekosa kabisa kujua nini ufanye baada ya mbinu zako za awali kukwama! Hatujaumbwa kushinda sisi Simba, ila kikosi tulichonacho hakistahili kufanya makosa ya mara kwa mara kama mchezo wa jana.
ReplyDelete