November 18, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amemkabidhi majukumu ya kuwafanyisha mazoezi ya viungo wachezaji wenzake Deogratius Munish 'Dida' baada ya kocha Adel Zrane kuondoka.

Dida amekabidhiwa majukumu hayo na kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems kutokana na Adel kurudi nyumbani kwao Tunisia.


Aussems alisema kuwa hakuna namna nyingine aliyoamua kwa sasa zaidi ya kumpa kazi Dida ili ashikilie jahazi hilo kwa muda.


"Adel amekwenda kwao kufanya mitihani yake ya chuo kikuu, kutokana na hali hiyo ndiyo maana unaona anawaoongoza wenzake kufanya mazoezi hayo," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic