November 18, 2018


Uongozi wa timu ya Yanga umesema kuwa watatumia mchezo wao wa kirafiki wa leo dhidi ya Namungo kujiandaa dhidi ya mchezo wao na Mwadui utakaochezwa Novemba 22.

Baada ya kucheza michezo 10 ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga wataanza kucheza michezo nje ya Dar.


Kaimu Katibu wa Yanga, Omary Kaya amesema kuwa mipango inakwenda sawa na watafanya vizuri ili kuhakikisha wanafanikiwa kuwa sawa hasa kwa michezo yao ya mikoani.

"Kila kitu kinakwenda sawa kwa upande wa maandalizi na tumejipanga kuhakikisha tunajiweka sawa maana baada ya kucheza michezo mingi Dar sasa tunaanza kutoka nje ya Dar, mashabiki watupe sapoti," alisema.


Kwa upande wa msemaji wa Namungo, Kidamba Namlia alisema wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo wao wa leo dhid ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic