Hatimaye familia ya mrembo wa Sudan ya Kusini aliyekuwa anagombewa na waposaji kibao walioahidi kutoa mahali kubwa zisizo za kawaida, ameolewa kwa mahari ya ng’ombe 520 na magari matatu aina ya Toyota V8!
Mrembo Nyalong Ngong Deng (17) kutoka eneo la Awerial, alikuwa na wachumba sita waliokuwa wanamtaka na kila mtu alikuwa tayari kutoa mahali bab’kubwa ikiwa ni pamoja na Sh. milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na Sh. milioni zipatazo 20 za Tanzania!
Akiwa amekaa kwa utulivu kando ya mumewe, tajiri mkubwa aitwaye Kok Alat katika ukumbi wa Freedom Hall jijini Juba, Ijumaa iliyopita, Novemba 9, Nyalong, mrembo wa kabila la Dinka, alikuwa nadhari ya mshangao uliowapata watu waliokuwa katika sherehe hiyo.









Duh!!!!Kali ya kufunga mwaka.
ReplyDeleteMtanzania anaangaika na mahai ya lak tano tena mke anakopeshwa na had anakufa mzigo hauishi....mtoto mwenyewe sasa!!!!!Hii ndio Sudan Kusini....kwetu huku warembo kama hawa wanapata tabu sana...na maneno ya wanaume
ReplyDeleteAngekuwa Tz huyu...kwanza angepigwa mimba alafu wazee wanakutana na maneno ya shombo "kama hamtaki laki mbili kaeni nae mtoto wenu".
ReplyDelete