Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm amesema kuwa anaona fahari vijana wake wanapopata matokeo ambayo anayahitaji hasa kwenye ligi kuu.
Azam FC imeendelea kutunza rekodi yake kwa kucheza michezo 13 bila kupoteza hata huku wakitoa sare michezo 3 na kushinda michezo 10 ya Ligi Kuu.
Pluijm amefichua kuwa anapata matokeo hayo kutokana na wachezaji kufuata maelekezo na kujituma ndani ya uwanja.
"Uwezo wao ni wa ajabu kwani wanatafuta matokeo kwa hali na mali, hilo ni jambo la kujivunia hasa kwa kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu.
"Bado tuna kazi ya kuendelea kutunza rekodi kwa kuwa kuna michezo mingi hasa ukizingatia timu zimeongezeka kwa sasa," alisema.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC izidi kuwa kinara wa ligi ikiwa na pointi 33 wakifuatiwa na Yanga ambao wana pointi 29.








0 COMMENTS:
Post a Comment