November 13, 2018


Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali ameibuka na kumpinga Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, George Mkuchika, ndani ya klabu hiyo kutokana na sakata zima la uchaguzi ambao unapaswa kufanyika mwezi Januari mwakani.

Akilimali ameeleza kushangazwa na maamuzi ya Mkuchika na Baraza lake kuingilia majukumu ya Kamati ya Utendaji ambayo ilikubaliana vizuri na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanyika kwa uchaguzi.

Mzee huyo amesema Baraza hilo halina mamlaka ya kubatilisha maamuzi ya TFF na Kamati ya Utendaji Yanga ambao walifikia makubaliano ya kujaza nafasi za viongozi Yanga ambazo hazina viongozi.

Akilimali amesema Yanga na TFF kwa pamoja walifikia mwafaka wa kumaliza kila kitu na kilichokuwa kimebakia ni kujaza nafasi sita pekee ikiwemo ya aliyekuwa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji.

Kutokana na malalamiko hayo, imeelezwa pia Akilimali amewataka TAKUKURU kufuatilia barua iliyosomwa na Mkuchika juzi akieleza kuwa na wasiwasi nayo inawezekana kukawa na namna.

Mumbe Akilimali ameitaka taasisi hiyo kuifuatilia barua hiyo ili kuweza kujipatia uhakika zaidi kwani haamini kama Manji ameituma na ikiwezekana kuna watu wanatumika ndani ya klabu.

6 COMMENTS:

  1. TFF na Serikali kupitia Wizara na BMT na akina Mzee Akilimali (na wanaomtumia) msiivuruge amani ya nchi kwa kuchochea vurugu....Sauti ya Umma na Sauti ya Wengi ni sauti ya Moyo....kama Wanachama wa Yanga (Bara na Visiwani) wanampenda, na wamesema, na wameridhia, na Yeye amejibu kwa maandishi, na wamefuata taratibu na kanuni zote za katiba yao....Wasikilizeni kwani ndio hali halisi lazima ukubali, uchaguzi ufanyike kwa kujaza nafasi za M/Mwenyekiti, wajumbe 4....kufanya kinyume na hapa....ni kumkosea sio tu wananchi bara na Visiwani....(kwani historia na sura halisi ya klabu hii inaakisi umoja wa Kiafrika....kwani sio th ndio klabu kongwe na ya kwanza kuanzishwa wakati ule wa Tanganyika 1935 mwezi 2)....bali pia Mungu....(kwani ni sauti ya wanyonge)

    ReplyDelete
  2. Serikali (Wizara & BMT) na TFF, na Mzee Akilimali mnaweza mkasababisha damu kumwagika......ni tahadhari....kwani hoja ya msingi ni kwamba kwanini Simba haiingiliwa? Kwanini Serikali, BMT na TFF mmekuwa PARTIAL KATIKA SUALA LA UCHAGUZI HAMKUFANYA HIVYO KWENYE UCHAGUZI WA SIMBA....ILA WA YANGA MMEUINGILIA???...Mnajenga chuki. na kuleta uhasama kwa mioyo ya watanzania wanyonge wanaoupenda mpira wa miguu (Yanga ina waasisi wa uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar....na ndio maana Wanachama wake wako imara sehemu hizi 2 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)....mke wa Hayati Karume kule Zanzibar ni mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini la Young Africans Sports Club)...kwa hiyo kugusa na kuivuruga klabu kama hii...ni kuchochea kuvurugika kwa utulivu na amani ya nchi. Nchi ina mambo ya msingi ya kujikita nayo kuliko kuiingilia matatizo ya vilabu vya Yanga na Simba....waacheni waendelee kama wanasema Mwenyekiti wao bado yuko madarakani....kwenda kinyume na hili kunasababisha maswali kulikoni huko????

    ReplyDelete
  3. Ni vema masuala ya Yanga yazungumzwe na Yanga, hakuna maana kuanza kuijadili Simba katika suala hili. Simba wamefanya uchaguzi na kumaliza kazi yao, kwa nini sasa mnabishana na wasimamizi wa soka? Uchaguzi tar 13 Januari 2019 na yeye ataingia ofisini tar 15 Januari 2019 hamuoni kama wanachanganya mafuta na maji?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  4. Huyu Akilima hana mapenzi ya dhati na Yanga anachofikiria yeye ni tumbo lake tu,wanachama wote was Yanga wameikubali ile barua ya Manji,yeye na kundi lake hawaitakii Yanga mafanikio

    ReplyDelete
  5. Sasa wewe unwmtisha nani eti damu itamwagika kamwage damu yako pumbavu unafikiri damu mchezo.

    ReplyDelete
  6. Hivi kumwaga damu ni kazi ndogo nini? Usizungumze kwa ajili ya kujifurahisha unamwaga damu kwa ajili ya nani au nini hasa? Maisha yako na maisha ya Yanga kipi ni bora? Usidanganye watu bwana!!!

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic