November 18, 2018

NA SALEH ALLY
YANGA inahitaji msaada kutoka kwa Wanayanga wenyewe, kwa kuwa hati yao hakuna anayeweza kukataa kwamba mambo ni magumu na kuna jambo linapaswa kufanyika.

Yanga ina hali ngumu kwa kuwa wachezaji hawajalipwa mishahara ingawa viongozi wamekuwa wakijitutumua kuonyesha kwamba kama vile mambo ni safi tu.

Tunajua, kwamba mambo si mazuri na huenda kipindi hiki wachezaji wamekuwa waungwana kupindukia na wavumilivu kupitiliza.

Itakapofikia siku wamechoka, basi wanapaswa kusikilizwa badala ya kuwalaumu kwa kuwa kwa sasa wako kazini lakini wanaendelea kucheza kama vile ni watu wanaojitolea.

Kitu kizuri zaidi kwao, wachezaji wa Yanga hawako katika nafasi mbaya pamoja na kuwepo kwa ugumu wa mambo ambao ni ukata.

Kwa sasa wanachokitafuta Yanga ni mtu wa kuwasaidia, mtu au watu wa kuwaondoa walipo na ndicho wanachokiangalia. Yeyote mwenye uwezo huo anaweza kuwa msaada.

Wanachama wa Yanga, zaidi wanamuamini Yusuf Manji ambaye amekuwa katika kipindi cha matibabu kwa muda sasa. Kuna jambo ambalo tunaweza kujifunza kutokana na nguvu kubwa inayotumika kumuondoa.

Naona nguvu kubwa kwa kuwa kuna mkanganyiko usio na sababu. Hivi karibuni wakati kamati ya uchaguzi ya TFF ilipotangaza, utaona kwamba ilifanyika hivyo ikiwa ni pamoja na kutangaza nafasi ya mwenyekiti, nayo ijazwe.

Wakati hali kama hiyo inatokea TFF, hakukuwa kuna barua nyingine ambayo ilitengua uenyekiti wa Manji kutoka TFF. Badala yake ipo ile inayomtambua kama Mwenyekiti wa Yanga huku ikisisitiza kwamba, Clement Sanga anapaswa kuvuliwa Uenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB).

Sanga alivuliwa uenyekiti wa bodi kwa maelezo kwamba wanachama wameandika kuwa wanaendelea kumtambua Manji sababu hawakuikubali barua yake ya kujiuzulu. Sasa kwani nani alimuondoa tena Manji madarakani?

Au ndiyo ile kauli kwamba alizungumza na Dk Harrison Mwakyembe na kusema yeye hagombei? Inawezekana ni utani au mazungumzo ya kawaida ambayo si ya kiofisi.

TFF imeitisha uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo bila ya kuwa imebadili uamuzi wake wa kumvua madaraka Sanga ambaye alionekana si mwenyekiti kwa kuwa mwenyekiti bado yuko madarakani kupitia uamuzi wa wanachama!

Sasa nani tena anakuwa na kauli ya juu kuzidi wanachama ndani ya klabu yao tena katika kitu walichokubaliana? Kama Manji aliwaomba wanachama kumsubiri amalizie matibabu, wao wamekubali, nani anawakatalia na kwa nini? 

Alisema atarejea kazini Januari na mwezi huo ndio TFF imepitisha ufanyike uchaguzi, tofauti iko wapi? Kuna jambo la kuliangalia.

Pamoja na hivyo, niwakumbushe kila sehemu kama ni TFF na hata serikali kuwa Yanga ni klabu ya Watanzania. Si lazima Manji aiongoze ndiyo itoke matatizoni, lakini kuna kila sababu ya kuheshimu mawazo na uamuzi wa wanachama wa klabu hiyo.

Kusikilizana ndilo jambo namba moja kwa watu wanaotaka kujenga jambo bora. Hivyo kama Manji anaondoka, vizuri kila utaratibu ufuatwe aende zake. Baada ya hapo Yanga iingie katika mchakato sahihi usio na walakini na kupata viongozi wao ambao wataungwa mkono na wanachama.

Nguvu kubwa sasa itumike kuikomboa Yanga katika eneo ililokwama badala ya kutaka kupambana na fulani asiwepo au asiingie. Kama kuna njia sahihi za kumuondoa, swadakta, zitumike ili kuondoa hewa ya hisia za uonevu.

Huko nyuma tumekuwa na mambo mengi ya figisu na yaliikwamisha michezo na hasa huu wa soka. Kwa sasa tunapaswa kujiepusha nayo kwa kiasi kikubwa ili kuwe na nafasi ya kujikita katika mawazo, mipango na utekelezaji wa maendeleo.
Bila Manji, Yanga inaweza kwenda. Uwazi wa mambo unaonukia haki, utatengeneza utulivu na uaminifu wenye lengo la kuendeleza soka na michezo kwa ujumla. Mtafakari.

12 COMMENTS:

  1. HEko,Wanaotaffuta nafasi yamanji ikwapuliwe Kwa lazima ni watu wanao chimba kaburi LA Yanga.usipate taabu kuwajua ziangalie tu rangi za tai zao.Tff ilisha mtambua Maji pale ilipo mvua madaraka yakemaka mwenyekiti Ndg Sanga.tff walitumia kanuuni kumvua Sanga.Je wanayo kanuni ya kumkataa Manji Leo au vitisho vyao vya kuwafungia watu ili waogope? Mfumo huu FIFA inauelewa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. acheni kuwa wapumbavu kiasi cha kujipa upofu na uziwi kilazima, TFF ilitengua wadhifa wa sanga pale TFF kutokana na maamuzi yao Yanga kwenye mkutano mkuu wao wa kujadili barua ya kujiudhuru wa Manji, lakini toka maamuzi hayo yachukuliwe Manji hajaanza kufanya kazi za yanga hadi leo na haonekani ana nia hiyo,sasa mnataka TFF ifiche ukweli kwa maslahi ya nani, kama Manji bado ana nia agombee tena au ajitokeze hadharani kusema bado yupo na lini ataanza kuwatumikia

      Delete
    2. Hiki ni mpja ya kipengele cha kwenye katiba ibara ya 28(3) Kimetaja Mjumbe wa Kamati ya Utendaji atakoma nafasi yake kwa sababu tofauti.
      Mjumbe atakoma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji iwapo atatenda au kufanya mojawapo ya mambo haya:
      (1)Kujiuzuru kwa maandishi na kuwasilisha barua yake ya kujiuzuru kwa Kamati ya Utendaji.
      (2)Hatahudhuria mikutano minne mfululizo a kawaida ya Kamati Kuu bila sababu ya msingi.
      (3)Anashindwa utekelezaji majukumu ya mjumbe kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo.
      (4) Anapatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa kufungwa bila mbadala wa faini.

      Delete
  2. mwandishi yupo sawa ila mnaopinga hampo sahihi hasa tukizingatia kua hiki ni kipindi cha dirisha dogo la usajili hivyo ni kuidhoofisha Yanga isiweze kusajili wachezaji wapya !! Yanga ni timu ya wananchi waachieni kiongozi wanayemtaka na si lazima Yanga iwe dhaifu ndipo yapatikane maendeleo kwa timu ya Simba !! hapo hamumkomeshi Manji wali wananchi wote wanaoishabikia Yanga !!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soma Katiba ya Yanga...*IBARAYA 29*
      Hii ibara inaelezea mambo matatu muhimu yanayohusu muda wa madaraka kwa viongozi wa Yanga mara tu baada ya kuchaguliwa.
      1.Muda wa Madaraka na Mamlaka ya Kamati ya Utakuwa wa miaka minne.
      2.Mamlaka ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji yanaweza kuongezewa muda .Hata hivyo ,mtu mwenye umri wa miaka 75 + hataruhusiwa kugombea Uenyekiti.
      3.Endapo itatokea kuwa nafasi yoyote ya Kamati ya Utendaji ya mjumbe kuwa wazi ,Kamati ya Utendaji itazijaza nafasi hizo za wazi mpaka Mkutano Mkuu wa Kawaida ujao ambapo nafasi zitajazwa kwa kuchaguliwa wajumbe wengine kwa kipindi kilichobaki cha Mamlaka.
      Katika ibara ya 28(3) Kimetaja Mjumbe wa Kamati ya Utendaji atakoma nafasi yake kwa sababu tofauti.
      Mjumbe atakoma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji iwapo atatenda au kufanya mojawapo ya mambo haya:
      (1)Kujiuzuru kwa maandishi na kuwasilisha barua yake ya kujiuzuru kwa Kamati ya Utendaji.
      (2)Hatahudhuria mikutano minne mfululizo a kawaida ya Kamati Kuu bila sababu ya msingi.
      (3)Anashindwa utekelezaji majukumu ya mjumbe kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo.
      (4) Anapatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa kufungwa bila mbadala wa faini.

      Delete
  3. Umeongea ukweli kabisaaa mwandishi wanaomzuia manji hawaipendi Yanga na nikudharau katiba na wanachama wa Yanga ambao ndiyo wenye timu yao mimi nawashauri TFF wawatendee haki yanga hata Kama wenyewe ndo wamiliki

    ReplyDelete
  4. Hata kama tff wana mamlaka wasitumie mamlaka hayo kwenye kuivuruga yanga demokrasia izingatiwe waiache yanga na timu yao

    ReplyDelete
  5. Matukio ya kukosa weledi, vitisho na propaganda za siasa michezoni hazitatusaidia kuvuka kimichezo kama Taifa bali tutavuna tulichokipanda. Ukikuta waliopewa dhamana za michezo wanapalilia migogoro jua hatuna nia njema na michezo kama tunavyochezea elimu. Baada ya Manji na Yanga nani atafuata? Tutie maji kichwani...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pitia katiba imeeleza kila kitu waandishi wanaandika ila vipengele vya katiba hawataki kuvinukuu..

      Hiki ni mpja ya kipengele cha kwenye katiba ibara ya 28(3) Kimetaja Mjumbe wa Kamati ya Utendaji atakoma nafasi yake kwa sababu tofauti.
      Mjumbe atakoma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji iwapo atatenda au kufanya mojawapo ya mambo haya:
      (1)Kujiuzuru kwa maandishi na kuwasilisha barua yake ya kujiuzuru kwa Kamati ya Utendaji.
      (2)Hatahudhuria mikutano minne mfululizo a kawaida ya Kamati Kuu bila sababu ya msingi.
      (3)Anashindwa utekelezaji majukumu ya mjumbe kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo.
      (4) Anapatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa kufungwa bila mbadala wa faini.

      Delete
  6. Kabla ya kuandika hii maakala umeisoma katiba ya Yanga?!Tuheshimu Katiba Tulizojitungia wenyewe
    *IBARAYA 29*
    Hii ibara inaelezea mambo matatu muhimu yanayohusu muda wa madaraka kwa viongozi wa Yanga mara tu baada ya kuchaguliwa.
    1.Muda wa Madaraka na Mamlaka ya Kamati ya Utakuwa wa miaka minne.
    2.Mamlaka ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji yanaweza kuongezewa muda .Hata hivyo ,mtu mwenye umri wa miaka 75 + hataruhusiwa kugombea Uenyekiti.
    3.Endapo itatokea kuwa nafasi yoyote ya Kamati ya Utendaji ya mjumbe kuwa wazi ,Kamati ya Utendaji itazijaza nafasi hizo za wazi mpaka Mkutano Mkuu wa Kawaida ujao ambapo nafasi zitajazwa kwa kuchaguliwa wajumbe wengine kwa kipindi kilichobaki cha Mamlaka.
    Katika ibara ya 28(3) Kimetaja Mjumbe wa Kamati ya Utendaji atakoma nafasi yake kwa sababu tofauti.
    Mjumbe atakoma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji iwapo atatenda au kufanya mojawapo ya mambo haya:
    (1)Kujiuzuru kwa maandishi na kuwasilisha barua yake ya kujiuzuru kwa Kamati ya Utendaji.
    (2)Hatahudhuria mikutano minne mfululizo a kawaida ya Kamati Kuu bila sababu ya msingi.
    (3)Anashindwa utekelezaji majukumu ya mjumbe kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo.
    (4) Anapatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa kufungwa bila mbadala wa faini.

    ReplyDelete
  7. Pia kuna ibara inaoelezea wanachama na maamuzi yao juu ya jambo la yanga tafuta lete uendelee kukalili kipengele kimoja na km kurudishwa na mkutano mkuu kungekuwa batili ujue TFF wasingemtoa Sanga jiulize kabla hujapotoshwa na vifungu vya Akilimavi,Saleh uko sahihi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic