November 19, 2018


Wakati kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jana kikiwa nchini Lesotho kusaka nafasi ya kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), imebainika kuwa, imetumia takriban Sh 31,669,440 kwa malazi pekee.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Championi ambalo limepiga kambi nchini hapa, kwa muda ambao kikosi hicho kimekaa Lesotho, kimetumia kiasi hicho cha fedha kwa malazi pekee.

Ipo hivi; timu hiyo ambayo awali ilipiga kambi nchini Afrika Kusini, ilitua Lesotho Ijumaa iliyopita na kukaa hapa Lesotho kwa siku tatu ambapo ilifikia kwenye Hoteli ya Avani ambayo ni ya kimataifa.

Kwa wastani, chumba kimoja bei yake ni randi 2,000 ambazo ni sawa na Sh 329,890. Kikosi kizima cha Taifa Stars kilichokuja Lesotho kina wachezaji 26 na viongozi sita wa benchi la ufundi. Jumla ni 32.

Idadi hiyo kwa siku moja,  walitumia Sh 10,556,480 kwa malazi ya kila mmoja kulala chumba chake. Kwa siku tatu ni Sh 31,669,440 kulala pekee.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic