VIDEO: YANGA WATOA MSIMAMO MWINGINE JUU YA MANJI KUTOCHUKUA FOMU
Mashabiki na wanachama wa yanga wameendelea kushikilia msimamo wao wa kumtambua Mwenyekiyi wao Yusuf Manji licha ya kutochukua fomu za kugombea nafasi hiyo.
Baada ya majina ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti kutangazwa na kamati ya uchaguzi ya TF F huku jina la Manji halipo, Global tv imezungumza na baadhi ya wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo juu ya msimamo wao kuhusiana na nafasi hiyo ya uenyekiti amabayo wanachama hawataki kuipigia kura
Yanga wanatarajia kufanya uchaguzi wao tarehe 13 January mwakani kwa mujibu wa kamati ya uchaguzi ya TFF kuziba nafasi zilizoachwa wazi na viongozi baada ya baadhi yao kujihuzuru akiwemo Mwenyekiti Manji.
Hata hivyo wengi wa wanachama wa yanga baado wanaamini kuwa nafasi ya mwenyekiti bado inashikiliwa na yusuph manji kufuatia barua iliosomwa na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa yanga ikidai manji atarudi klabuni hapo January 15 mwakani.








TFF BMT na Wizara husika ya michezo wanacheza mchezo wa kuangamiza soka si Yanga pekee pasipo kujua ama kusudi. Hivi TFF walipomng'oa Sanga na kumtambua Manji kama Mwenyekiti wa Yanga walikuwa ulevini? Je wakati huo hayo yakitokea BMT na Wizara husika walikuwa usingizini?
ReplyDeleteJe yule Kiongozi aliyesema wanaisaidia sana Yanga kwanini bado wachezaji wanadai mishahara ya miezi kadhaa? Tuendeleze siasa katika michezo gharama zake tutazionq tu.
Huyo manji kama kweli anaipenda timu why hajitokezi kusema? Hivi yanga haiwezi kuendelea bila manji? Acheni fikra potofu wana yanga, chagueni viongozi wa kujenga misingi ya uwekezaji yanga si kutegemea pesa za mifukoni mwa watu
ReplyDeleteHuyo manji kama kweli anaipenda timu why hajitokezi kusema? Hivi yanga haiwezi kuendelea bila manji? Acheni fikra potofu wana yanga, chagueni viongozi wa kujenga misingi ya uwekezaji yanga si kutegemea pesa za mifukoni mwa watu
ReplyDeleteYanga ilikuwepo na itaendelea kuwepo bila Manji.Kulikuwa kuna matajiri ambao wameicha Yanga kuendelea kuwepo kina Sheriff Shiraz,Abbasi Ghulamali,Viran na wala hawakuwa viongozi na walifadhili klabu lkn wameiacha Yanga.Kuna kipindi mwishoni mwa miaka 1975 kulitokea mgawanyiko Yanga raizon na kandambili.MzeeTabu Mangara (mwenyekiti) na matajiri kina sheriff Shiraz walijiondoa Yanga na kwenda kuanzisha Pan Africa na waliacha Yanga na ikabaki kuwa Yanga hadi leo.Swala hapa ni kuwapa somo kuwa usimtegemee mtu au kikundi fulani bali kutengeneza mfumo ambao hautaegemea kwa mtu mmoja ili maisha yaendelee.
ReplyDeleteKuna wakati tutajielewa japo ni mbali kusubili kujielewa.
ReplyDelete