YANGA YAMPATA MBADALA WA MANJI, HUYU HAPA
Baadhi ya wanachama wa Yanga wamejitokeza na kumtaka Abbas Tarimba kugombea nafasi ya uenyekiti ndani ya klabu hiyo.
Wanachama hao baadhi wamesema Tarimba ndiye mtu pekee ambaye anastahili kuchukua nafasi ya Yusuf Manji endapo hatojitokeza kugombea nafasi hiyo.
Tarimba ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Yanga na kuanzisha suala la kuibadili klabu hiyo kuwa kampuni anapigiwa upatu wa kugombea nafasi hiyo.
Tayari Shirikisho la Soka Tanzania limeshapanga tarehe ya kufanyika uchaguzi huo ambao utakuwa Januari 1 2019.
Uchaguzi huo utasimamiwa na Kamati za Uchaguzi mbili ambazo ni ile ya TFF kwa mujibu wa BMT na Yanga wenyewe.








Tarimba anautaka wenyekiti na genge lake
ReplyDeleteYanga inahtaji mtu mbunifu na si mwenye hela nyingi. Kiongozi sahihi ni yule atayejua nini cha kufanya kwa mfano...lazima tuwe na afisa masoko, anayeweza kuingia mikataba sahihi kwa ajili ya Maslahi ya timu...mpiganaji atakaeweza kuifanya Yanga iwe na uwanja wake wa mechi na si mazoezi angalau wenye kuingiza watu elfu 20. Mpango mwingine ni kuwa na Afisa Mipango ambae atajua muelekeo mzima wa timu kwa miaka wastani 5. Afisa Mipango ndio mratibu wa kiofisi kuhusu mfumo mzima wa uendeshaji na bajeti nzima kwa kuwa atapokea uendeshaji wa timu kwa mwaka mzima kutoka kwa Meneja, Kocha na timu ya uongozi. Ndoto za Abbas Tarimba zilikuwa nzuri kipindi kile na ndio timu nyingi hata za Ulaya zinapokimbilia. Kama atahitaji kuwa kiongozi sidhani kama kuna shaka ila lazima tupate timu ya uongozi bora na bila kuweka mtu kufata maslahi binafsi
ReplyDeleteTarimba ni mtu sahihi kuiongoza Yanga.
ReplyDelete