ZAHERA APINGANA NA HOJA YA MABAO MENGI YANGA, HAYA NDIYO ALIYOFUNGUKA
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameibuka na kupingana na baadhi ya wadau wa soka wanaohoji kwanini timu yake haifungi mabao mengi.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya mechi kadhaa zilizopita kikosi cha Yanga kushindwa kufunga mabao mengi kwenye michezo yake.
Zahera amesema kuwa wao wanachokiangalia ni ushindi na kupata alama tatu pekee ili kujiwekea nafasi nzuri za kutwaa ubingwa.
Mkongomani huyo ameweka wazi kuwa ligi ni ngumu na ina mechi nyingi hivyo amewaasa wale wote wanaozungumzia mabao mengi ni vema wakazingatia alama tatu kwanza.
Yanga itakuwa kibaruani kesho kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na Ndanda FC ya Mtwara.








yanga ndoo tunabeba kama matani
ReplyDeleteLabda kama mechi zote watachezea dar na sio kwa ushindi wa goli moja na kwa kucheza kwa kupaki basis hata kwa time kama alliance
Deleteni vyema kukiri kuna tatizo katika kikosi chako, sio kusema tunachoangalia ni ushindi na alama tatu sasa kama wanasawazisha hilo goli point tatu unapataje, kubali tu kikosi kina tatizo .basi tutakuelewa,
ReplyDeleteAnasema eti "ligi ni ngumu na ina mechi nyingi", sasa hii inaweza kuwa sababu ya kufunga kigoli kimoja?. kama ni ngumu kwani hizo timu zinazoshinda magoli mengi zinacheza ligi ya wapi! si zinacheza ligi hiyo hiyo ambayo wewe unasema ni ngumu!. Tatizo unaongea sana utadhani wewe ndiye msemaji wa timu. Ifikie hatua ujikosoe makosa yako. Kubali madhaifu mzeee, timu yako inaonekana imeishiwa mbinu za kuuzidi uwezo wa timu pinzani. Ingia darasani tena mzee. Taifa ukipata gori moja ujue kuna mkwakwani, Kambarage, Nangw'anda, Samora, na juzi umeuona uwanja utakaoenda kucheza na Biashara; tambua kule utapigwa au kama utajitahidi basi ni sare tasa.
ReplyDelete