December 12, 2018



Kocha wa African Lyon, Adam Kipatacho amesema kuwa hana taarifa na wachezaji ambao hawajaripoti katika timu ila anaamini ataungana nao akirejejea Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na michezo yake ijayo ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Yanga.

Kipatacho amesema kuwa walipata sare ya kutofungana kwa kuwa kuna wachezaji ambao bado hawajajiunga na timu yake kwa sasa ila anajipanga kwa ajili ya michezo ijayo.

"Mbao ni timu imara hasa ikiwa nyumbani wanafanya vizuri ndio maana tukaja kwa tahadhari kubwa hivyo tunajipanga kuweza kupata matokeo katika michezo yetu ijayo dhidi ya Ndanda, Yanga," alisema.

Baadhi ya wachezaji ambao hawapo na timu ni pamoja na Haruna Moshi ambaye amekuwa ni msaada kwenye timu kutokana na uzoefu wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic