Beki mpya wa Simba, Zana Coulibaly ambaye ni raia wa Burkina Faso, amewekwa kando kwa muda ili kupewa muda wa kuzoea mazingira ya timu.
Beki huyo ambaye amesajiliwa hivi karibuni akitokea klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast ni mbadala wa Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa beki huyo kwa sasa hayupo kwenye mipango yake hivyo hana muda wa kuhangaika naye.
"Zana yupo hapa anafanya mazoezi na wenzake ila sihangaiki naye sana kwa kuwa hayupo kwenye mpango katika mchezo wetu dhidi ya Nkana FC, hivyo nimemuacha na wenzake ili aweze kuzoeana nao na usajili wake ukikamilika tutakuwa naye katika kazi," alisema.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteKocha wa Simba ni very professional tofauti na Zahera wa Yanga. Zahera kweli anaendelea kupata matokeo mazuri lakini anaongea hovyo. Hizo sifa anazopewa kuwa anawaambia ukweli wachezaji hadharani ni za kijinga kwani anaweza tu atatumia busara na akaeleweka vyema na wachezaji wake bila ya mipasho. Siamimi kama hakuna wachezaji wanaomkwaza Ausems wa Simba lakini hatujawahi kumsikia akiwananga wachezaji wake. Tumemsikia Triple C akimuelezea kocha wake kuwa jinsi anavyoishi na wachezaji kama vile baba mwenye upendo na familia yake. Hakuna kocha aliekuwa ana uwezo wa kunyanyua uwezo wa mchezaji mmoja mmoja hata atakuwa mkorofi kwa miaka ya hivi karibuni kwenye ligi ya bongo kama uwezo aliekuwa kocha wa Simba Patrick Phiri wa Zambia na kwa kweli ni vigumu kuisikia kauli ya Phiri hata akikwazika.
ReplyDeleteWatanzania wengi wanapenda kuongopewa. Wakiambiwa kwel mnabisha. Kama mzazi akificha makosa yako utaendelea kuwa mjinga milele. Tuendelee kusutana
ReplyDelete