Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm amesema kuwa hana presha ya kushindwa kuishusha Yanga kileleni kwa kuwa bado ligi inaendelea.
Azam wamecheza michezo 16 na wamefanikiwa kushinda michezo 12 na kutoa sare michezo 4 wakiwa wameachwa pointi 1 na Yanga ambao wapo kileleni na pointi 41 huku wao wakiwa na pointi 40.
Pluijm amesema katika mchezo wake dhidi ya KMC matokeo aliyopata ya sare sio mabaya kwani vijana wa KMC walitambua wanakutana na timu bora hali iliyofanya wajiandae vizuri.
"KMC walijua aina ya timu ambayo wanakutana nayo hivyo hesabu zao zikawa ni kuzuia na kushambulia, wamefanikiwa kutufunga nasi pia tumewafunga hivyo wote tumepata pointi 1 sio mbaya kwetu.
"Kuhusu kuweza kuwa kileleni hilo ni jambo la wakati kwa kuwa malengo yetu hayawezi kuyumbishwa na mtu tutasimamia kile ambacho tunaamini na tutapambana ili kupata matokeo katika michezo yetu ijayo hilo linawezekana," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment