December 12, 2018




Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Heritier Makambo mwenye mabao 8 amevunja mwiko wa kushindwa kufunga kipindi cha pili katika michezo ya Ligi kuu alioufungulia uwanja wa Taifa baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Makambo mwenye mabao 8 kwa sasa alifanikiwa kufunga mabao 7 kwenye Ligi Kuu yote akifunga kipindi cha kwanza na kwa kutumia zaidi mguu wa kushoto kufunga mabao yake manne na 3 alifunga kwa kichwa.


Katika mchezo wa Yanga dhidi ya Biashara United, Makambo alifunga bao la 2 dakika ya 80 kwa mguu wa kulia katika uwanja wa Taifa na kumfanya avunje mwiko wake.


Mabao ya nyuma ambayo Makambo alifunga kipindi cha kwanza ni dhidi ya Mtibwa Sugar dk 30, Coastal Union dk 10, Lipuli dk ya 9, JKT Tanzania dk ya 19, Mwadui dk ya 10, Kagera Sugar dk ya 22 na Alliance FC dk ya 18 hivyo bao lake dhidi ya Biashara United limevunja mwiko huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic