Uongozi wa Yanga umesema kuwa unatambua uwezo wa Kiungo mahiri wa timu ya African Lyon ambaye alikuwa pia ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania hivyo na kuwataka mashabiki wasiwe na mashaka watatoa tamko kuhusu kuitumikia timu hiyo.
Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kila kitu ni mipango na kuna utaratibu wa kufuata hivyo hakuna haja ya kuwa na papara.
"Tunatambua uwezo wa Boban si mchezaji wa kubezwa hata kidogo hivyo umuhimu wake ni mkubwa na anakipaji cha mpira, kuhusu kujiunga na timu yetu bado dirisha lipo wazi hivyo tutaweka wazi kila kitu baada ya muda," alisema.
Usajili wa Boban Yanga umeonekana kuwashtua mashabiki wengi kutokana na taarifa za ndani kueleza kwamba amesajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili kukitumikia kikosi hicho, dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Desemba 15.
0 COMMENTS:
Post a Comment