Mashabiki wa Simba, wamelazimika kuchelewa kuondoka mjini Kitwe kutokana na matengenezo ya basi lililowapeleka.
Basi la Simba, lililokuwa limewabeba mashabiki na baadhi ya waandishi wa habari, lilipata ajali karibu kabisa na mji wa Kitwe.
Hadi leo asubuhi, bado matengenezo yalikuwa na yanaendelea na ilielezwa ilikuwa ni hatua za mwisho za matengenezo hayo.
Taarifa nyingine zilieleza, mashabiki hao wanaweza kuondoka mchana huu au jioni.
Kama isingekuwa tatizo hilo, mashabiki hao walipanga kuondoka alfajiri ya leo kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Simba ilicheza na Nkana FC na kupoteza mchezo wao kwa kufungwa mabao 2-1 na sasa wanasubiri mchezo wa pili jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment