December 16, 2018



Hatimaye basi lilowabeba mashabiki wa Simba, limeanza safari kutoka mjini Kitwe, Zambia kurejea jijini Dar es Salaam.


Basi hilo lilipata ajali na mashabiki hao wakalazimika kusubiri baada ya muda waliopanga kuondoka kwa kuwa basi hilo lilikuwa katika matengenezo.

Baada ya matengenezo hayo ya "kuegesha" ili matengenezo kamili yaje yafanyika jijini Dar es Salaam, basi hilo limeanza safari hilo ndefu.


Basi la Simba, lililokuwa limewabeba mashabiki na baadhi ya waandishi wa habari, lilipata ajali juzi karibu kabisa na mji wa Kitwe.


Hadi leo asubuhi, bado matengenezo yalikuwa na yanaendelea na ilielezwa ilikuwa ni hatua za mwisho.



Kama isingekuwa tatizo hilo, mashabiki hao walipanga kuondoka alfajiri ya leo kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.


Simba ilicheza na Nkana FC na kupoteza mchezo wao kwa kufungwa mabao 2-1 na sasa wanasubiri mchezo wa pili jijini Dar es Salaam.a

2 COMMENTS:

  1. Mungu awafikishe salama 🚒

    ReplyDelete
  2. Polen Mashabiki Wa UKweli Wa Simba Kwa Changamoto Hiyo Iliyo Wapata Naamini Mtafika Tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic