December 23, 2018


Kocha Msaidizi wa timu ya Azam FC, Juma Mwambusi amesema anatambua ugumu wa kupata matokeo kwa timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kutokana na kukamia kupata matokeo hali inayomfanya awe na tahadhari kubwa.

Azam FC leo anacheza na Madini FC ikiwa ni mchezo wa kombe la Shirikiso utakaochezwa uwanja wa Chamazi majira ya saa 1:00 Usiku.

"Ugumu wa timu ndogo ni mkubwa kwa kuwa hawatabiriki wakiwa uwanjani, wana mbinu kali za kutafuta matokeo, tumejipanga kufanya vizuri na tumewapa tahadhari wachezaji wetu katika mchezo wetu," alisema.

Azam FC wanacheza leo ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa raundi ya tatu na mshindi atakayepatikana anasonga hatua ya mbele atakayefungwa anayaaga leo mashindano rasmi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic