December 23, 2018


Washambuliaji wa kimataifa wa timu ya Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wamesema hawana wasiwasi na mchezo wao wa leo dhidi ya Nkana FC ya Zambia, ahadi yao kubwa kwa mashabiki ni kupambana kufa na kupona.

Simba wataumana na Nkana FC ya Zambia saa 10:00 jioni ukiwa ni mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ule wa kwanza waliocheza Zambia kukubali kipigo cha mabao 2-1.

Kagere amesema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kutokana na maandalizi ambayo wameyapata wana imani ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao.

"Ushindani ni mkubwa nasi tumejipanga kupata matokeo na hilo linawezekana kutokana na morali ambayo tunayo hasa na tutacheza kwa ushirikiano kutafuta matokeo," alisema.

Okwi amesema mashabiki wanapaswa wajitokeze kwa wingi leo Taifa kuwapa sapoti katika mchezo wao ambao ni mgumu ila wapo tayari kupata matokeo.

"Kupata matokeo na kushinda ni hesabu zetu hasa kwenye mchezo wa kimataifa, ni kufa na kupona leo hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi leo," alisema.

Simba leo wanahitaji ushindi wa bao 1-0 ili kuweza kuvuka hatua ya kwanza na kuingia kwenye makundi wakishindwa kupata matokeo watatupwa kwenye hatua ya Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic