Leo ilichezwa droo kwa ajili ya kupanga makundi ya mchezo huo, ambapo KMC itakuwa nyumbani katika uwanja wa Uhuru kuikaribisha Tanzania Prisons.
Ofisa habari wa KMC, Anwar Binde amesema anatambua ugumu wa michuano hiyo kutokana na ukubwa wa mashindano ila wana imani ya kufanya vizuri kwa kuwa kocha ana uzoefu na wachezaji wanaimarika kila siku.
"Uwepo wa mashindano haya kwetu ni somo pia tunakutana na timu yenye uwezo ambayo inashiriki ligi kuu, uzoefu wa mwalimu wetu, Ettiene Ndayiragije utatufanya tupate matokeo," alisema.
Bingwa wa mashindano haya anapata fursa ya kuiwakilisha nchi katika mashidano ya kimataifa ambapo kwa sasa ni Mtibwa Sugar ambaye anashikilia ubingwa huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment