December 18, 2018


Kocha Mkuu wa KMC, Ettiene Ndayiragije amesema anatambua ubora wa kikosi cha Simba ila anaamini mbinu alizowapa wachezaji wake watapata matokeo.

KMC watashuka dimbani kesho uwanja wa Taifa kuvaana na mabingwa watetezi Simba wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 5-0 katika mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa uwanja wa Uhuru.

"Simba ni timu imara na bora kwetu tunaamini ni kipimo kizuri kwa wachezaji wetu hasa kwenye ligi ambayo ina ushindani, tupo tayari kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo wetu.

"Mbinu mpya ambazo nimewapa wachezaji wangu naamini zitasaidia kupata matokeo na tunachohitaji ni pointi tatu katika mchezo wetu, ushindani uliopo unatufanya tuweze kukomaa zaidi," alisema.

KMC wamecheza michezo 16 na wanashika nafasi ya 9 baada ya kufikisha jumla ya pointi 21 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic