December 18, 2018


Uongozi wa Simba umesema kuwa utabadilisha kikosi kitakachovaana na wapinzani wao KMC kesho katika uwanja wa Taifa ili kuwapa nafasi wachezaji wengine kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Nkana FC ya Zambia.

Simba kesho wanakibarua cha kucheza na KMC katika mchezo wa ligi kuu ikiwa ni kiporo chao kutokana na kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema wanatambua wana kazi nzito ya kutetea ubingwa na kuweza kusonga mbele kwenye hatua ya makundi hivyo wamejipanga kuweza kupata matokeo.

"Tuna kazi ya kucheza na KMC kesho, tunawaheshimu wapinzani wetu na tunatambua ushindani uliopo ila tumejipanga kupata matokeo katika mchezo huo na tutabadili kikosi chetu.

"Tutawapa nafasi wachezaji wetu kwenye kikosi ili wengine waendelee na maandalizi dhidi ya Nkana FC ya Zambia, sapoti ya mashabiki ni muhimu katika hili," alisema.

6 COMMENTS:

  1. Ngj wafungwe ili yanga atangazwe bingwa mapema

    ReplyDelete
  2. Alafu waachage ujinga sasa wakikosa ligi kuu alafu kimataifa ndo wata chemsha

    ReplyDelete
  3. Simba msifanye mchezo mkasema wachezaji wengine mukawaweka upande kwakusema mkazo zaidi kwa nkana kwasababu mkiukosa ubin. Mnakutana na Nkana kwakuwa nyie ni mabingwa, jee mkiukosa ubingwa vipi vipi mtaweza kukutana nao tena ikiwa Nkana au timu uoyote huko mbeleni bila ya ubingwa na mjue KMC si timu nyepesi

    ReplyDelete
  4. Kweli tupu ndugu tusije kuyakosa yote tukaondoka kote. Huwwzi kuingia ndani ya chumba bila kupitia mlangoni

    ReplyDelete
  5. bora mfanye hvyo maana wapinzan wetu wapo kwa ajili ya kutusoma.

    ReplyDelete
  6. Lakini pia sijui hili nalo TFF hakuluiona au!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic