Kocha wa timu ya Lipuli, Seleman Matola amesema kikubwa kinachowafanya wapate matokeo kwa sasa ni kutengamaa kwa kikosi chake ambacho amekaa nacho kwa muda mrefu na kutoa onyo kwa timu nyingine.
Lipuli yenye maskani yake Iringa, jana ilifanikiwa kuishushia kipigo cha mabao 9-0 timu ya Laela katika mchezo wa Shirikisho uliochezwa uwanja wa Samora.
"Hatuna tatizo ndani ya timu, tayari wachezaji wameshazoeana hasa baada ya kukaa kwa muda mrefu na kufanya tuwe na muungano mzuri, hilo ni jambo ambalo linatufanya tuwe na nguvu na morali ya kutafuta matokeo kwa kila timu tutakayokutana nayo," alisema.
Bingwa wa kombe la Shirikisho anapata fursa ya kuiwakilisha nchi kimataifa, ambapo mtetezi wake Mtibwa Sugar jana alitolewa kwenye mashindano ya kimataifa baada ya kufungwa na timu ya KCCA ya Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment