WAWILI WAPIGWA STOP SIMBA HUKU MMOJA APEWA NAFASI
Mabosi wa juu wa klabu ya Simba wamewapiga STOP wachezaji wake, John Bocco na Emmanuel Okwi kuondoka kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kitaifa, imeelezwa.
Taarifa imeeleza kuwa Bocco anawindwa na timu kutoka Misri huku Okwi akiwaniwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Licha ya kuhitajika kwao kwa kipindi hiki, uongozi Simba umetia ngumu kwani wanatakiwa kuipa timu nguvu kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ukiachana na uongozi, Kocha Mkuu Mbelgiji, Patrick Aussesm naye amewataka mabosi wake kutowauza wachezaji hao kwakuwa bado anawategemea na anaamini mchango wao bado unaonekana.
Mbali na wawili hao, Adam Salamba naye kuna hatihati ya kubakia kikosini kwani amekuwa akiwinda na timu kadhaa za nje lakini uongozi umesema unaliangalia hilo ikiwezekana anaweza akaondoka.
Uwezekano wa Salamba kuuzwa upo kutokana na kutotumika zaidi katika kikosi cha kwanza hivyo yawezekana akauzwa kwenda klabu nyingine ili kuendeleza kiwango chake.
Taarifa za ndani zinasema Salamba amekuwa akihitajika Ubelgiji nchi ambayo Mbwana Samatta anachezea soka lake, hivyo endapo suala lake litaiva anaweza akaondoka.
Duh! Okwi Na Bocco Nahisai Ndo Simba Yenyewe Na Wameleta Tofauti Ya Simba Ile Ya Kawaida Na Kuwa Simba Hatari Nashukuru Uongoz Na Kocha Kwa Kuliona Hilo Wasubirie Dirisha Kubwa Ili Wakitoka Tupate Mbadala Wao
ReplyDeleteBocco bora wamruhusu
ReplyDelete