Rais Dkt John Magufuli, leo Desemba 23, anapokea Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania. Ndege hiyo itawasili leo majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege.
0 COMMENTS:
Post a Comment