Zuberi Maeda (19) mkazi wa Kiterini, Moshi alibahatika kuibuka kuwa mshindi wa droo ya 71 ya promosheni ijulikanayo kama Shinda Zaidi na SportPesa inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa.
Timu ya SportPesa ilifika mpaka jiji la Moshi kwa ajili ya kumkabidhi kwani mpaka kukabidhiwa bajaji yake mshindi hapaswi kutumia kiasi chochote cha fedha.
Akizungumza wakati wa makabidhiano Bwana Zuberi alisema “Kupata bajaji hii kutakuwa kumetatua sana matatizo yangu kwa maana nina bustani ya mboga mboga, nitakuwa nikiifanyia biashara huku nikihudumia shamba langukwa maana nilikuwa nampango wa kuanza biashara ya mifugo.”
Nategemea kuwa mfanyabiashara mkubwa hapo baadaye na namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa maana kupitia bajaji hii ndoto zangu zitatimia, nitaanza kufuga kuku wa kisasa au wa mayai na kutunza faida wakati bustani yangu na bajaji vikiniingizia kipato hadi pale nitakapoanza kujitengenezea faida kubwa ili nifungue biashara kubwa” alisema Zuberi.
Baba mzazi wa Zuberi bwana Saidi Zuberi Maeda alisema ” Nilivyosikia mwanagu kashinda kiukweli sikuamini, nilifurahi sana hadi nilishindwa kula, kwa sababu mwanangu kama mnavyomuona kuwa ni kijana mdogo mwenye ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa kupitia miradi mbalimbali, kupitia bajaji hii ninaimani haya mambo yatakamilika”
“Nimejisikia vizuri mjukuu wangu kujishindia bajaji hii kwakweli, nikiugua nitakuwa na uhakika wa usafiri wa kunipeleka hospitali pamoja na babu yake, sasa huyu mjukuu wangu ndiyo miguu yangu na tumepata ahueni kama familia” alisema Bi Chausiku Zuberi ambaye ni Bibi wa Zuberi Maeda.
Kutoka SportPesa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania alisema Zuberi ni kijana mdogo sana na kama kampuni tumefurahi kuona anajishindia bajaji itakayomuwezesha kubadili nakuinua maisha yake kiuchumi.
“Familia yake inamtegemea na ikiwa anandoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa tungependelea kumuona baada ya mwaka mmoja amepiga hatua kwani uwezo huo anao na kitendea kazi ambacho ni bajaji.”
“Promosheni yetu bado inaendelea na ningependa kuwahamasisha watumiaji wa mitandao yote ya simu yani (Zantel, Tigo, Vodacom, Airtel pamoja na Halotel) kupitiahuduma zao za kuhamisha fedha kupitia simu ya mkononi wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka SportPesa.
“Kucheza piga namba * 150 *87# na uweke pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa ili kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo Jezi ya Simba na Yanga pamoja na tiketi ya kwenda Uingereza na Hispania kuangalia mechi za ligi hizo zinazoendelea” alisema Tarimba
0 COMMENTS:
Post a Comment