Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema maumivu ya kupoteza mchezo wao wa kimataifa katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya Nkana FC yatalipwa katika uwanja wa nyumbani kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.
Simba walikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Nkana FC ambayo mtanzania Hassan Kessy anaitumikia katika mchezo uliochezwa uwanja wa Nkana uliopo nchini Zambia.
"Tuna kazi kubwa na ngumu ya kuweza kupata matokeo kwa kuwa lengo letu ni moja kuweza kusonga mbele katika michezo ya kimataifa, hilo linawezekana kwa kuwa wenzetu walifanikiwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani nasi kazi yetu tunaweza.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa katika mchezo wetu wa marudiano utakaochezwa uwanja wa Taifa, kwa kufika kwenu tutapindua matokeo kibabe na kutimiza malengo yetu ya kusonga mbele katika mashindano ya kimataifa," alisema.
Mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi katika michuano hiyo na ili Simba waweze kufuzu wanahitaji kushinda bao 1-0 kwenye mchezo wa marudio utakaochezwa jumapili kwa kuwa wanafaida ya bao la ugenini.
Jamani Mmeilewa Mbinu Aliyomaanisha Hapa! Ni Ya Kuisapoti Simba Uwanjani Taifa Kama Kawaida Yetu Simba Tukaujaze Uwanja Wa Taifa Lazima Nkana Wata Ogopa Tu Wakiwa Ktk Hali Ya Kushangaa Uwanja Na Mashabiki Wale Ma 3 Ya Fasta Warudi Kwao Porini Huko Kitwe
ReplyDeleteyap!tutaenda kuujaza,simba nguvu mj.
ReplyDeleteSIMBA
ReplyDeletenguvu moja,
simba nguvumoja
ReplyDeleteSimba nguvu moja
ReplyDeleteKwapamoja tunaweza.
ReplyDelete