December 17, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema wanaombeza mchezaji wake mpya Haruna Moshi 'Boban' wataisoma namba uwanjani kutoka kwa mchezaji huyo ambaye ametokea timu ya African Lyon.

Boban amemwaga wino kuitumikia Yanga kwa muda wa miezi sita kwa dau la shilingi milioni ishirini na tano ili aweze kuongeza nguvu ya kusaka ubingwa katika kikosi cha Yanga ambacho kwa sasa hakishikiki kwa kuwa kinaongoza ligi kikiwa na jumla ya pointi 44.

"Wapo ambao wanabeza juu ya uwepo wa Boban ndani ya Yanga, acha wasubiri wakati ukifika watajihukumu wenyewe, ni mchezaji mzuri mwenye akili ya mpira akiwa uwanjani ana uwezo wa kumiliki na kulinda mpira jambo ambalo ni nadra sana kwa wachezaji wengi kufanikiwa kufanya hivyo." alisema.

Yanga wamesajili wachezaji wawili dirisha dogo ambao ni Boban pamoja na Ibrahim Hamad ambaye ni mlinda mlango na wamewatoa wachezaji wanne ambao ni Pato Ngonyani, Said Mussa (African Lyon) Yusuf Mhilu (Ndanda) na Emmanuel Martin (Ruvu Shooting).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic