December 18, 2018




Uongozi wa Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba umefunguka kuwa beki wake wa kati Salum Mbonde amerejea kikosini na sasa ameanza kufanya mazoezi mepesi baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akismbuliwa na majeraha.

Mbonde alitua Simba akitokea Mtibwa Sugar msmu uliopita ila amekumbana na bahati mbaya kwa kuwa toka ametua klabuni hapo hajapata muda mzuri wa kucheza baada ya kupata majeraha ya goti kwenye mechi ya Simba dhidi ya Lipuli iliyopigwa msimu uliopita Uwanja wa taifa.

Akizungumza na Waandishi wa habari za michezo makao makuu ya klabu hiyo msemaji wa mabingwa hao wa tanzania bara Haji Manara amesema kuwa hali ya Mbonde imeanza kuimarika na tayari ameshaanza kufanya mazoezi mepesi akijiandaa kurejea kikosini kwenye dulu ya pili ya ligi kuu msimu huu.

"Mbonde anaendelea vizuri na tayari ameshaanza kufanya mazoezi mepesi mepesi ili kujiweka sawa kurejea rasimi kikosini kwa ajili ya kuendelea kuipambania klabu yetu,nafikiri mungu akijalia kheri tutamuona Uwanjani muda siyo mrefu," alimaliza Manara  


2 COMMENTS:

  1. Mungu mfanyie wepesi jembe letu arudi kazini kwani pengo lake ni kubwa sana klabu!Kila la kheri MBONDE

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic