Kikosi cha Nkana Fc 'The Devil' inatarajia kutua leo usiku kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ikitokea kwao Zambia tayari kuwakabili Simba Jumapili hii kwenye mchezo wa marejeano kwa vilabu bingwa Afrika.
Nkana ambayo inatumikiwa na mchezaji wa kitanzaia Hassan Kessy inatua kucheza mchezo huo wa marudiano ikiwa tayari na mtaji wa ushindi wa bao 2-1 waliouvuna kwenye mchezo wa kwanza waliocheza wakiwa nyumbani wiki iliyopita.
Ofisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara ameliweka wazi ujio wa wapinzani hao kuja kuwakabili Simba alipozungumza na waandishi wa habari za michezo kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mitaa ya msimbazi kariakoo,huku akiweka wazi kuwa timu hiyo itatua nchini kwa kutumia usafiri wa shirika la ndege la Kenya.
"Nkana FC wataingia leo usiku wakitokea kwao Zambia kuja kuwakabili Simba kwenye mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika na watakuja kwa usafiri wa shirika la ndege la Kenya,kwahiyo leo usiku ndiyo watatua pale Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere," alisema Manara.
Kama Nkana wanakuja leo na kesho Simba anacheza mechi ya ligi basi ni kumrahisishia kazi Nkana. Na yawezekana wanakuja mapema ili kuiwahi hiyo mechi ya ligi kati ya Simba na KMC. Kweli Simba anapaswa kucheza viporo vyake vya mechi lakini sioni kama busara katikati ya wiki hii Simba kucheza mechi ya ligi kabla ya mechi ya maamuzi itakayoamua nani atasonga mbele katika club bingwa Africa.
ReplyDeleteNaamini benchi la ufundi lina mkakati na mipango ya ushindi bila kujali wanatazamwa na Nkana
ReplyDeleteHii ni kuinyepesisha mechi kwa KMC. Ila naamanini watakaopewa nafasi ya kucheza hii leo, watajua ni nini nafasi yao kwa upande wa Simba.
ReplyDeleteSimba ndiyo timu pekee inayowezo kucheza mechi mbili kwa wakati mmoja na zote ikapata matokeo ya ushindi hapa Tanzania alisema msemaji wa club ya Simba ndugu Haji Manara.
ReplyDelete