December 25, 2018


Ili kuziba pengo la Emmanuel Okwi, tetesi zilizo chini ya kapeti zinasema kuna uwezekano mabingwa watetezi wa ligi kuu bara, Simba kumsajili kiungo mshambuliaji matata wa Nkaa Red Devils, Walter Bwalya.

Bwalya ambaye aliwapa wakati mgumu Simba haswa mabeki wake katika mechi mbili walizokutana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ananukia kutua Msimbazi ili kuchukua nafasi ya Okwi ambaye anatajwa kusajiliwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Tayari taarifa za Okwi kuondoka Simba kwa mujibu wa mtandao wa Kawowo Sports wa Uganda, zinasema mchezaji huyo ameshamalizana na timu hiyo.

Kuondoka kwa Okwi kutawafanya mabosi wa Simba kuanza kugharamika na Nkana juu ya usajili wa Bwalya kwa kutegemeana na mkataba wake ulivyo.

Simba hivi sasa ipo katika maandalizi ya mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika, SportPesa Super Cup, Kombe la FA na Mapinduzi CUP huko Zanzibar.

8 COMMENTS:

  1. Hilo galasa linasubiri mipira ifike miguuni

    ReplyDelete
  2. Ndio zenu...mnaandika habari za udaku ili watu wasome..hata asante kotoko walivyokuja dar mshambuliaji wao rastav tuliandikiwa eti anakuja simba...Phfewww hata makambo anakuja simba

    ReplyDelete
  3. Yule kiungo wa Mbabane keshakuja ? Au hii ni blog ya udaku?

    ReplyDelete
  4. Ni kawaida kuwepo kwa tetesi za usajili na mwisho klabu ndio inayoamua Nani asajiliwe kulingana na mahitaji na Mambo mengine. Ni haki ya waandishi kutupa tetesi hizo na duniani kote ndivyo ilivyo, so don't get bored guys!

    ReplyDelete
  5. Viongozi na benchi la ufundi la Simba hasa kocha ndie mwenye maamuzi ya nani wa kuja kiziba pengo la Okwi. Naweza kusema hivi sasa sina mashaka na watu wa usajili pale Simba wanaonekana wapo vizuri ila umakini unatakikana katika kuziba pengo la Okwi ikiwezekana ni kutafuta mchezaji mwenye uwezo zaidi ya Okwi. Ukiangalia Okwi hakuwa katika kiwango chake cha kawaida kwenye hizi mechi mbili za Nkana ni kama alikuwa mtu mwenye mawazo labda hilo la kwenda Kaiser chiefs au labda anaona ufalme umevamiwa na Triple C na kujikuta kelele za Okwi haziimbwi tena sana kama za Chama,Chama,Chama. Na kama ni hivyo basi SIMBA ni wamuache tu aondoke kwa amani kwani tunaimani viongozi wa Simba wana uwezo wa kumleta mchezaji mwenye uwezo zaidi ya Okwi kama usajili bado unaruhusu ila binafsi ningewashauri viongozi wa Simba kutoacha kupambana kutafuta sign ya Mbukinafaso wa Asante kotoko Sogne kama bado yupo kwenye fomu kwani ni zaidi ya Bwalya na pengine zaidi ya okwi.

    ReplyDelete
  6. Na kuhusu mbombo Vipi? Wanasema ni mkali kuliko Bwalya

    ReplyDelete
  7. Kasi ya Walter Bwalya imepungia sana. Sio Bwalya yile aliyetakiwa na Simba misimu miwili iliyopita. Simba watafute mchezaji mwenye uwezo mkubwa zaidi kuliko Okwi ili aungane na Chama kuleta maangamizi kwa timu pinzani.

    ReplyDelete
  8. Wote Mmetoa Maoni Mazuri Namm Namalizia Kwa Kuukubali Uongozi Mpya Wa Simba Na Jinsi Ulivyo Makini Kusajiri Ni Imani Yangu Atakaye Chukua Nafasi Ya Okwi Si Kiongera Wala Selenkuma Danny Bali Ni Mtu Mwenye Uwezo Wa Hali Yajuu Kumzidi Okwi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic