Mabingwa wa soka Tanzania, Simba wametua salama mjini Kitwe nchini Zambia tayari kuwavaa Nkana FC.
Nkana FC watakuwa wenyeji wa Simba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa mjini humo Jumamosi.
Simba imewasili mjini Kitwe ikiwa na kikosi kizima tayari kwa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.
Mchezaji wa zamani wa Simba, Hassan Kessy ni kati ya wachezaji tegemeo wa kikosi cha Nkana FC ambayo ni moja ya timu kongwe za nchini Zambia.
Kessy aliondoka Simba na kujiunga na Yanga ambayo mwishoni haikumsajili na yeye kuamua kusaka timu nchini Zambia.
Kila la kheri chama langu. Nawaamini.
ReplyDelete