SIMBA WATUMA SALAAM YANGA, WAAHIDI UBINGWA LIGI KUU
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Simba umesema hakuna wa kuizuia kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu licha ya kuwa haipo juu ya kilele cha msimamo wa ligi.
Katika msimamo wa ligi, Simba imechacheza jumla ya mechi 12 ikiwa na alama 27 wakati Yanga ambayo haijapoteza hata mchezo mmoja ikicheza mechi 16 na ikiwa na alama 44.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Haji Manara, ameeleza kuwa walio juu wamekaa kwa muda pekee kwa maana wao nguvu zao wameziwekeza kwenye mashindano ya kimataifa.
Manara amewatambia watani zake wa jadi, Yanga kuwa wajiandae kushuka muda wowote pale watakaporejea rasmi kwenye ligi kutokana na hivi sasa wamebanwa na mechi za kimataifa.
"Suala la kutetea ubingwa wa ligi kwetu halina hata mjadala, kuna watu wamekaa pale juu wakishikilia nafasi zetu, ni suala la muda tu, tutarejea na tutaikalia hapo baadaye" alisema Manara.
Simba leo inashuka dimbani kucheza na KMC katika kipute cha ligi, kusaka alama tatu za kabla haijavaana na Nkana Red Devils ya Zambia kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment