December 19, 2018


Kiungo fundi kutoka Congo, papy Kabamba Tshishimbi amerejea kwao baada ya kupatwa na msiba wa baba mkwe wake.

Kwa maujibu wa Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, amesema Tshishimbi tayari ameshasafiri kuelekea kwao na hatakauwa sehemu ya mchezo wa kesho dhidi ya African Lyon.

Tshishimbi ambaye ni moja ya wachezaji tegemeo Yanga, ameondoka na kukifanya kikosi hicho kizidi kupungukiwa na makali kuelekea mechi hiyo ya ligi.

Ukiachana na Tshishimbi, Yanga pia itawakosa wachezaji wengine dhidi ya Lyon ambao ni beki Andrew Vincent na Rafael Daud ambao ni majeruhi.

Saleh amesema wawili hao bado hawajawa fiti na imewapelekea kubakia Dar es Salaam wakati kikosi kikisafiri kwenda Arusha tayari kwa kipute na Lyon.

Yanga itashuka majira ya saa 10 kamili kesho kukipiga na Lyon kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

1 COMMENTS:

  1. Ukiandika KWA MUJIBU WA... huandiki tena AMESEMA...
    Badilikeni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic